Sunday, September 22, 2013

KAMERA YETU WEEK END HII IMEANGAZA MNADANI MAGUGU

 Ilikuwa mapema Jumamosi ya wiki hii kwenye mji mdogo wa  Magugu Babati Vijijini ambapo wafugaji, wakulima, wafanyabiashara/wajasiriamali na wananchj kutoka vijiji mbalimbali vya Mkoa wa Manyara, mikoa/wilaya karibu kama Arusha, Kondoa n.k walikutanika kwenye mnada  kijijini hapo kwa madhumuni ya kuuza na kununua mifugo, mazao na bidhaa mbalimbali. Mnada ulikuwa umechangamka, bidhaa za kutosha na idadi kubwa ya watu.
 Angalia kwenye picha.....
Sagulasagula ya nguo ikiendelea, wateja wakijinunulia  nguo kwa bei poa kabisa

Kama ilivyokuwa kawaida kwenye minada/magulio ya aina hii  kitu cha nyama choma hua akikosekani, pichani mdau mmoja kama alivyobambwa na camera yetu akingojea nyama ziive.


Wadau hawa walikutwa na canera yetu wakitafuna nyama choma kwenye moja la banda la mamalishe ama mama pima kama wanavyojulikana kwenye baadhi ya  maeneo

Friday, September 13, 2013

Sugu na shauri lake la kumdunda askari polisi Bungeni bado

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu (Chadema) ambaye anatuhumiwa kumjeruhi Askari wa bunge jana hakufikishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa huku Jeshi la polisi likisema linaendelea na upelelezi.
Mbunge huyo jana aliripoti Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Dodoma kutokana na tuhuma zinazomkabili za kumjeruhi Askari wa Bunge.
Mbilinyi anadaiwa alimpiga kichwa pamoja na ngumi na kumjeruhi  jicho la upande wa kulia Koplo Nikwisa Nkisu.
Aliripoti  makao makuu ya polisi kama alivyopangiw huku akiwa ameambatana na wakili wake ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Akizungumza mara baada ya kuripoti kituoni hapo, Lissu alisema polisi wanaendelea na upelelezi na  watawasiliana nao baada ya wiki mbili.
Kwa mujibu wa Lisu Jeshi la polisi limesema linaendelea na upelelezi na watatoa taarifa lini watakuwa tayari ikiwemo maamuzi watakayochukua kama kuendelea na kesi au la.
Hata hivyo alisema atashangaa kama polisi watafungua kesi kwa sababu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Ibara ya 100 (2), inaeleza Mbunge hatashitakiwa au kufunguliwa jinai lolote kwa jambo atakalofanya au kusema ndani ya Bunge, hii inamaanisha katika viwanja vyote vya Bunge.
Alisema anamshangaa Naibu Spika Job Ndugai kwa  kupigia kelele suala hilo liende wanaopiga kelele hili jambo liende mahakamani.
Lisu alisema kisheria Sugu hawezi kushtakiwa na kwamba kinachofanyika ni mashinikizo ya watawala.
Kwa upande wake Sugu alisema kinachofanyika sasa kinatokana na alichokiita uhuni wa Ndugai.
Alisema kilichotokea bungeni kilikuwa ni maagizo ya Ndugai kwa kuwa alisikika akisema huyo Sugu anajifanya mjanja mtoeni nje akome.
Alisema  vitendo vyao havijatukatisha tamaa, tutakomaa, hatuogopi sio tu kupigwa bali hata kuuwawa kwa kutetea maslahi ya umma.
Sakata hilo la Sugu lilitokana na vurugu zilizotokea katika ukumbi wa Bunge baada ya wabunge wa kambi ya upinzani kupigana hadharani na askari wa Bunge.
Wabunge hao walichapana ndani na nje ya ukumbi, hali iliyosababisha tafrani kubwa, huku maofisa usalama na askari polisi kutoka kituo kikuu mjini Dodoma, wakilazimika kuitwa kwenda kuongeza nguvu ili kukabiliana na hali hiyo.
Vurugu hizoo zilizuka baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kunyanyuka ili kutaka kutoa hoja, ambapo Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alimtaka kukaa chini hali iliyowafanya wabunge wote wa upinzani kunyanyuka wakiashiria kumuunga mkono.
Katika vurugu hizo ‘Sugu’ inadaiwa alimpiga kichwa pamoja na ngumi na kumjeruhi  jicho la upande wa kulia Koplo Nikwisa Nkisu.
Aidha chanzo cha vurugu hizo  ni madai ya wabunge kutoka vyama vya Chadema, CUF  na NCCR- Mageuzi kutaka kuahirishwa kwa muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuwa mchakato wa kuandaliwa kwake haukuwashirikisha Wazanzibar.