JESHI la Polisi Mkoani
Dodoma linawashikilia watu wanane kwa kukutwa
na madawa ya kulevya aina
ya bangi na mirungi pamoja na zana za
kufanyia uhalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) David
Misime alisema kukamatwa kwa watu hao kunatokana
na msako unaoendelea wa
kupambana na wahalifu na uhalifu uliofanyika
eneo la Chang'ombe Machi
11, mwaka huu.
Katika msako huo Polisi
waliwakamata watuhumiwa hao wakiwa na kilo
moja na misokoto 104 ya bangi, mirungi gram 500 zana za kuvunjia
yakiwemo mapanga, mikasi,
visu na nondo.
Kwa mujibu wa Kamanda
Misime msako huo ulihusisha zaidi kero za
uvutaji wa bangi na
kupelekea kufanya uhalifu katika maeneo
mbalimbali Manispaa ya
Dodoma.
Aliwataja waliokamatwa
kuwa ni Halfan Muheza (25), Stewart Sylvester
(18), Shaban Ibrahim
(18), Abdallah Idd (18), Fikiri Jonas (20), Ally
Nuru (30), Saimon Zabron
(43) na Albert Charles (18) wote wakazi
Chang'ombe Manispaa ya
Dodoma.
Kamanda Misime alisema
watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani leo
kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Pia alisema Jeshi la
Polisi linaendelea kumtafuta Dereva wa gari
linalosemekana kuwa ni
Toyota Land Cruiser GX Standard rangi nyeupe
baada ya kumgonga mpanda
baiskeli aliyefahamika kwa jina la Julias
Sanduku (50) Mkazi wa
Gairo katika eneo la Kijiji cha Visimi Kibaigwa
na kumsababishia kifo
mpanda baiskeli huyo.
Alisema dereva huyo
alikuwa akitokea Dodoma kuelekea Morogoro baada ya
kumgonga mpanda
baiskeli,alishuka kutoka ndani ya gari na kumwangalia
aliyemgonga alipogundua
amefariki akageuza gari kurudi njia ya Dodoma
na kuwaambia wananchi
waliojitokeza kuwa anaenda kutoa taarifa jambo
ambalo hakufanya.
Kamanda Misime aliwaomba wananchi wenye
taarifa na dereva huyo alipo
wajulishe katika kituo
chochote cha Polisi ili aweze kukamatwa.

No comments:
Post a Comment