Na Mwandishi wetu
TANZANIA inapoteza jumla ya shilingi bilioni 301
kila mwaka kama gharama ya kukabiliana na madhara ya uchafu wa mazingira.
Hayo yalisemwa jana na Meneja wa Mradi wa Usafi wa
Mazingira Tanzania (UMATA), Kornel Kema wakati akizungumza kwenye mafunzo kwa
waandishi wa habari juu ya usafi wa mazngira iliyofanyika Dodoma.
Huku akinukuu ripoti ya Benki ya Dunia ya Programu
ya Usafi wa Maji na Mazingira iitwayo ‘Madhara ya Kiuchumi yatokanayo na hali
duni ya usafi wa mazingira afrika’, Bw. Kema alisema kuwa fedha hizi ni nyingi
na kwamba zingeweza kuokolewa kama usafi wa mazingira ungeboreshwa nchini.
Kwa mujbu wa ripoti hiyo, jumla ya Watanzania milioni 26 wanatumia vyoo duni na pia zaidi ya
watu milioni tano hawana choo na kwamba wanajisadia haja ndogo na kubwa kwenye
maeneo ya wazi.
Pia inaonesha kuwa mtu mmoja asiye na choo bora
hupoteza muda wa siku mbili na nusu kwa mwaka katika kutaafuta eneo la
kujisadia katika maeneo ya wazi ili watu wengine wasimuone.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na mradi wa UMATA
yalifunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa.
Kwa mujibu wa Mkwasa alisema pamoja na kwamba Dodoma
ina matatizo makubwa ya upatikanaji wa maji lakini hilo lisiwe kisingizio cha
kutotiliaa maanani usafi wa mazingira.“Hatuwezi kuacha wananchi wasijali usafi kkwa vile kuna tatizo la maji , usafi wa mazingira si kuoga tu ni usafi wa jumla katika kaya na hata kuhakikisha kuna choo bora” alisema
Mradi huo unafadhiliwa na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usafi wa Mazingira (GSF) na kutekelezwa na Shirika la Plan International katika wilaya za Bahi, Chamwino na Kongwa mkoani Dodoma.


No comments:
Post a Comment