MKAZI
wa wa kijiji cha Chibwechangula –Behelo katika
Wilaya ya
Mpwapwa Mkoani Dodoma, Ruth Matonya (26) amejifungua mtoto wa ajabu
ambaye nusu ya sura yake ilikuwa ikifanana na binadamu na nusu
ikifanana na chura.
Mtoto huyo alizaliwa Desemba 2, mwaka huu katika Kituo cha Afya cha
Mtakatifu Luka kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya
Mpwapwa. Ambapo alifariki dakika chache baada ya kuzaliwa.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dk. Edwin Kihura mara
baada ya mama huyo kufika kituo hicho cha afya alikuwa na uchungu
mkali ambao uliendelea bila kukoma na baadaye alishindwa kujifungua
kwa njia ya kawaida licha ya kuwa njia ilikuwa imefunguka.
Alisema kutokana na hali hiyo ilimazimika mama huyo kufanyiwa upasuaji
ili kuweza kuokoa maisha yake na mtoto.
Alisema wakati mama huyo akihudhuria kliniki walipojaribu kupima
miezi ya mwisho mama huyo lakini mkao wa mtoto ulikuwa haupatikani,
wala mapigo ya mtoyo yalikuwa hayapatikani lakini mtoto alikuwa
anacheza tumboni jambo ambalo lilikuwa likiwashangaza sana waganga na
manesi kituoni hapo.
Dk. Kihura alisema mara baada ya mama huyo kufanyiwa upasuaji
waliweza kutoa mtoto wa jinsi ya kike ambae alikuwa na sura isiyo
eleweka na kichwa kilikuwa nusu na sura ya binadamu na nusu ikiwa ni
sura inayofanana na chura lakini viungo vyake vyote vikiwa kamili.
Alisema zipo sababu kadha ambazo zinazoweza kusasabisha tatizo kama
hili ambapo alisema kuwa ni baadhi ya akina mama kukosa baadhi ya
madini mwilini na uumbaji kuto kamilika ambao unasababishwa na sababu
za kibailojia ambazo ni kushidwa kugawanyika kwakromozome.
Alisema tatizo hilo kitaalam linajulikana kama Anecephaly.
Pia alisema matatizo kama hayo huweza kutokea mala chache sana katika
hospitali nyingi lakini vitendo hivi vimekuwa vikiongezeka kwa wingi
kwa siku za hivi karibuni .
Alisema hali ya mama huyo inaendelea vizuri na pia huyo alikuwa ni
mtoto wake wa tano.

No comments:
Post a Comment