MKUU wa mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi amekitaka Chuo Kikuu cha Dodoma
kutumia taasisi yake ya Confucius (CIUDOM) kufunza watanzania utamaduni na
tabia za china kwa lengo la kuwawezesha watanzania kutumiakikamilifu fursa
za kiuchumi zilizopo China kwa kujiamini na kujinafasi.
Dk Nchimbi alitoa kauli hiyo juzi wakati wa tamasha linaloambatana na
sherehe za mwaka mpya wa Kichina kwa mujibu wa kalenda ya taifa hilo.
Mwaka mpya wa Kichina mwaka huu umeadhimishwa Januari 27 kwa mujibu wa
kalenda iliyozoeleka.
Pamoja na kupongeza chuo hicho kwa kuandaa sherehe hiyo, mkuu huyo wa mkoa
alisema kwamba amefurahishwa sana na kuwapo na sherehe hizo ambazo
zinakumbusha pia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na China.
Dk Rehema ambaye alielezea kuridhishwa kwake na UDOM kupitia taasisi yake
ya CIUDOM kwa kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho
katika kuwatamadunisha watanzania, aliwataka watanzania kutumia nafasi
zilizopo UDOM kujifunza lugha ya kichina na utamaduni wake ili kukabiliana
na fursa za kiuchumi za taifa hilo kubwa duniani.
Alisema kwa kujua lugha ya kichina na utamaduni wake watanzania watakuwa na
nafasi ya kushiriki moja kwa moja katika uchumi wa China na kujipatia
manufaa makubwa.
Alisema wananchi wa Tanzania wanastahili kutumia uwapo wa taasisi
inayofunza masuala ya China ili kujiongezea maarifa kutokana na ukweli kuwa
uchumi wa China unazidi kukua na Tanzania ina nafasi katika ushiriki wake.
Naye makamu mkuu wa chuo Profesa Idris Kikula alisema katika hotuba yake ya
kumkaribisha mkuu wa mkoa kwamba, Chuo hicho kimeingia matapatano ya
kuanzishwa kwa taasisi ya Confucius ikitambua kuwa ni nyenzo muhimu kufikia
ustawi wa watanzania.
Alisema katika kutambua uchumi wa China , urafiki uliopo na hali ya baadae
ya wafanyabiashara wa Kitanzania kwa kuzingatia shughuli nyingi za kiuchumi
zinazofanywa na China kusaidia maendeleo nchini China, UDOM pamoja na
kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzisha wa CIUDOM pia iliandaa tamasha
hilola majira ya michepuo China kuenga kuungana na wachina katika
kusherehekea mwaka mpya na pia kujifunza mambo kutoka kwa raia wa China
waliopo nchini.
Katika mahojiano baadaye kuelezea maana yake, Profesa Kikula alisema kwamba
ifikapo mwaka 2030 China itakuwa nchi yenye uchumi mkubwa pengine kuliko
taifa lolote lile duniani, na kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa, mengi ya
mataifa yatakuwa yanafanyabiashara na China na watanzania hawastahili
kukosa nafasi kutokana na ukaribu uliopo kati ya mataifa hayo mawili tangu
enzi za awamu ya kwanza ya uongozi baada ya Uhuru wa Tanzania.
Ni dhahiri katika hili kuwepo kwa taasisi inayofundisha nadharia za
Confucius kutasaidia kuiandaa Tanzania kufanya biashara kisahihi na China.
Kwa maneno yake mwenyewe profesa Kikula anasemaa kuanzishwa kwa taasisi
hiyo ni maandalizi ya kuwafanya watanzania washiriki kikamilifu katika
uchumi wa dunia ambao kufikia mwaka 2030 ni dhahiri utatawaliwa na China.
Alisema kuufahamu utamaduni wa China na lugha yao kutasaidia hata kuondoa
uwezekano wa kutapeliwa na wajanja wachache ambao wanatumia watanzania
kutoelewa lugha ya Kichina katika masuala ya biashara.
Katika kujifunza utamaduni wa Kichina kupitia nadharia za Confucius
watanzania wanapata nafasi ya kujifunza utamaduni wa kichina uliowawezesha
kuwa na uchumi mkubwa katika kipindi cha muda mfupi. Aidha watajifunza
busara mbalimbali ambazo zikitumiwa zinaweza kutengeneza mfumo wa maisha
ambao pia utawanyanyua watanzania kifikira na kuwafanya wajitume maradufu.
Wachina wanaamini kwa mujibu wa mafundisho ya Confucius mtu akishindwa
lengo, dawa si kubadili lengo, bali kubadili njia au vitu vinavyosababisha
kushindwa ili kulifikia lengo husika.
Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dodoma (CIUDOM) kilizinduliwa rasmi
Aprili 28,mwaka jana na makamu wa rais Dk Mohammed Ghalib Bilal.Kuanzishwa
kwa CIUDOM kumeifanya tanzanuia kuwa moja ya nchi zenye taasisi zipatazo
400 za Confucius zilizotapakaa duniani kote.
Katika tamasha hili kikundi cha sanaa cha China cha Henan Art Troupe
kilifika na kuwatumbuiza wageni na wananchi wlaiohudhuria tamasha hilo.
mwisho
No comments:
Post a Comment