![]() |
| malecela akizungumza leo nyumbani kwake |
WAZIRI Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), John Samwel Malecela amemtaka Mbunge wa Monduli Edward Lowasa
kuacha kuanza mbio za urais kabla ya wakati kwani anakiuka misingi ya katiba ya
Chama.
Alisema hayo leo wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika nyumbani kwake Kilimani Mjini Dodoma ambapo pia alionesha fulana ambazo zimekuwa zikisambazwa nchi nzima zilizoandiwa 'Friends of Edward Lowassa.
"Chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na kujiuliza fedha wanatoa wapi? Na hayo madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani huku Watanzania
wakiendelea kuwa maskini" alisema Malecela wakati wa mkutano huo.
Malecela ameitaka Sectretatieti ya CCM kumjadili Lowasa
kutokana na vitendo hivyo kwa sasa ni kukiuka misingi ya katiba ya chama.
Alisema anamuuanga msemaji wa UVCCM),Paul Makonda kwa kitendo chake cha kumkemea Lowasa bila uoga kwa jinsi anavyokivuruga chama kwa lengo la kutaka Urais 2015 huku sekretarieti ikiwa kimya.
"Hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani
ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi, mpaka tumuachie mtoto ndiyo akemee hayo hapa chama kipo wapi?" alihoji Malecela
Alisema vijana wanachama wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais bila mafanikio.
"Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudi za viongozi wa sasa wa chama ngazi za juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu Abdulahaman Kinana na Katibu Mweneze Nape Nnauye za kutetea chama zinatiwa mchanga" alisema.
Alisema vijana wanachama wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais bila mafanikio.
"Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudi za viongozi wa sasa wa chama ngazi za juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu Abdulahaman Kinana na Katibu Mweneze Nape Nnauye za kutetea chama zinatiwa mchanga" alisema.
Alitaka juhudi zao zisibezwe na watu wenye nia njema na chama kwani wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama kwa wananchi kila pembe ya taifa kwa kukemea na kuelezea misingi ya
uongozi bora.
"Sisi tulikijenga chama hiki kwa tabu sana na hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka, nidhamu na busara na uchungu wa raslimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndiyo
vilivyotuongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na Serikali.
"Wakati wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi ya katiba amekamekemea tabia ya baadhi ya watu ndani ya chama walioanza kuonyesha nia ya kuutaka urais kwa kutumia fedha zao
kinyume na misingi na katiba ya chama.
Mbali na hilo amesema kuwa wakati watu hao wakifanya hivyo, sekretarieti ya chama hicho imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio za urais bado.
Akizungumzia suala la malumbano ndani ya chama, alisema kuwa vitendo hivyo havijana tija kwa chama.
Alisema hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juuwamejibishana kwenye vyombo vya habari, vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani ya
chama kwa muda mrefu,"
"Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu Makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta kutoelewana ndani ya chama kusiko
kuwa na lazima,"alisema Malecela.
Akijibu maswali kwa waandishi baada ya kuuliza kukemea Lowasa peke yake wakati kuna wengine wanaofanya hivyo, Malecela alisema kuwa yeye hawajui hao wengine anamjua Lowasa na kuingia ndani na kutoa fulana mbili moja ikiwa na rangi nyeusi na kahawia na nyingine yenye rangi
nyekundu na nyeupe zikiwa zimeandikwa 'Friends of Edward Lowasa'.
nyekundu na nyeupe zikiwa zimeandikwa 'Friends of Edward Lowasa'.
Malecela alisisitiza kuitishwa kwa kikao cha
sekretarieti ili kutafakari jambo hilo ili litafutiwe dawa.
Hata hivyo alisema hawezi kulizungumzia suala la mawaziri mizigo kwani ni mambo yaliayoanzia bungeni nab ado yanaendelea kuzungumzwa. Alisema hata enzi za TANU watu walikuwa wakiokota maneno ya kusambaza na lile.
Alipoulizwa kwa nini akiwa kama mjumbe wa baraza la ushauri la CCM amekabiliana vipi na suala hilo, Malecela alijibu kuwa ameongea kama John Samwel Malecela ambaye amekuwa makamu mwenyekiti wa CCM kwa miaka 15 na anaongea kama mwanachama mwenye uchungu na nchi yake.."Baraza limeundwa chini ya Ibara ya 127 ya katiba ukisoma utaona nini kazi ya baraza, ina nguvu gani na inaelekeza kufanya nini" Alihoji
Malecela


No comments:
Post a Comment