Thursday, December 18, 2014

Kongwa ni zaidi ya uzuri ina historia ya kipekee


.Baadhi ya makaburi wa wapigania uhuru wa Nchi za Msumbiji, Afrika Kusini na Zimbabwe yaliyo katika Wilaya ya Kongwa.

WILAYA ya Kongwa ilianza kujulikana katika ramani ya dunia mwaka 1913 kutokana na Shirika la kidini kutoka Canada lililojulikana kama Church Missionary Society (CMS) kujenga Chuo cha Ualimu na Theolojia katika Kijiji cha Mlanga mwaka 1909.
Pia Kongwa ilipata umaarufu baada ya vita kuu ya pili ya dunia ambapo Shirika moja la kilimo la Uingereza lililojulikana kama Overseas Food Cooperation kuanzisha utafiti wa kilimo cha karanga .
Hata hivyo mwaka 1949 wilaya hiyo ilifutwa kutokana na kushindwa kwa mradi wa karanga hali iliyosababishwa na ukosefu wa mvua kwa miaka mitatu mfululizo jambo lililolazimu Shirika la Oveseas kufunga shughuli zake.
Kabla ya Uhuru Wilaya ya Kongwa ilikuwa ikiongozwa na Watemi au Machifu wa makabila ambao ndio walikuwa wanatawala maeneo mbalimbali kwa kurithishana.
Mtemi Nuyanji alitawala eneo la Pandambili, Mtemi Mahinyika akitawala Kongwa, Mtemi Kasawa alitawala Mlali na mtemi Simango alitawala eneo la Sagara.
Hata hivyo baada ya Tanzania kupata uhuru, mfumo machifu ulibadilika na kuwa mfumo wa  kidemokrasia ambapo jamii husika ilikuwa ikichagua kiongozi waliyemtaka.
Wakazi wa Kongwa ni Wagogo, Wakagulu, Warangi na makabila mengine ambayo yalihamia kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania kama Wabena, Wanguu, Wangoni, Wakamba na Wamasai ambao walifika hapo kwa  ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.
Kwa Mujibu wa Mkuu  Wilaya ya Kongwa, Alfred Msovella,Wilaya ya Kongwa ilianza mwaka 1996 chini ya sheria ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982.
Wilaya hiyo ina ukubwa wa eneo la kilomita 4,041 ambapo eneo linalofaa kwa kilimo na ufugaji ni hekta 363,690 ambapo wilaya ina tarafa tatu za Kongwa, Mlali na Nzoisa, kata 22, vijiji 87, miji midogo miwili ya Kongwa na Kibaigwa.
Mwandishi wa makala haya akitoka ndani ya handaki lililotumiwa na wapigania uhuru wa Msumbiji.

Kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 na kwa kuzingatia ongezeko la watu la asilimia 2.4 katika mwaka 2014 wilaya hiyo inakadiriwa kuwa na jumla ya wakazi 324,296
Unapofika katika kambi ya wapigania uhuru iliyopo katika Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma utaona ni jinsi gani Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere alivyojitoa na kutoa ardhi ya Tanzania ili itumike kama njia ya ukombozi kwa Nchi nyingine za Afrika.
Unapozungumza na watu mbalimbali wanaeleza jinsi baba wa T aifa alivyoamua ardhi ya Kongwa na Tanzania kwa ujumla itumike kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi ili nchi zipate uhuru na kuutokomeza ukoloni na ubaguzi wa rangi.
Nafika kwenye kambi hiyo, najionea nyumba ambayo aliwahi kuishi Rais wa kwanza wa Msumbiji Samora Machel na hata nyumba aliyowahi kuishi Rais wa kwanza wa Namibia Sam Nujoma.
Japo baadhi ya majengo ya kambi hiyo yamekuwa yakitumika kama shule, majengo mengine yanaonekana kuanza kubomoka na kutishia kupotea kwa historia hiyo ambayo inaweza kutumika kama njia ya kujifunza japo kuna watafiti kutoka mataifa mbalimbali wamekuwa wakitebelea kambi hiyo kujifunza.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kongwa, White Zuberi anasema, alisema wilaya hiyo ina historia pana kutokana na kuwa na kambi ya ukombozi ya wapigania uhuru wa Afrika.
Kwa Mujibu wa Mwenyekiti huyo wa halmashauri kambi hiyo ilijengwa mwaka 1964 ambapo wapigania uhuru kutoka nchi za Msumbiji, Angola, Zimbabwe, Namibia na Afrika kusini walikuwa wkiishi kawenyr kambi hiyo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Alfred Msovella
Pia kuna nyumba ambazo walikuwa wakiishi Samora Mashel abaye alikuwa Rais wa kwanza wa Msumbuji na sam Nujuma Rais wa Namibia.
Zuberi anasema wliomfahamu Sam Nujoma wakati huo, walisema alifiia hatua ya kuongea hata kidogo.
“Alipokuwa akipita kijijini walikuwa wakimsalimia Mlimswano- kwa maana ya habari gani kwa kigogo lakini Nujoma alikuwa akidhani walikuwa wakimuuliza habari za Chama cha ukombozi cha Namibia Swapo ambalo kinaelekea kufanana na salamu hiyo” anasema
Lakini alipofahamu kama hiyo ni salamu akawa akiitikia kam salamu lakini alijua kiasi lugha ya kigogo kutokana na kukaa na watu wa Kongwa kama ndugu.
Baada ya kambi hiyo kufungwa kutokana mwa wapigania uhuru hao kuondoka miaka ya 1980 majengo hayo yakachukuliwa na Jeshi na yalitumika mpaka mwaka 1995  yakaanza kutumika kama shule ya sekondari ya Kongwa.
Pia Mkuu wa majeshi wa sasa Davis Mwamnyange aliwahi kuwa mkuu wa kambi hiyo ambayo wakati huo ilikuwa Kambi ya Maafisa Usalama wa Jeshi.
Aidha kuna makaburi ya wapigania uhuru hao ambao walifariki wakati wakiwa kwenye kambi hiyo na waliozikwa na wanajeshi kutoka Namibia, Afrika kusini na Msumbiji.
“Hata viongozi wa nchi hizo na ndugu wa marehemu hufika kutembelea makaburi hayo na kuyasafisha, huwa tunapokea wageni wengi tu kila mwaka” anasema
Hata hivyo anasema sasa wanafanya mazunguzo na serkali ili eneo hilo liwe la makubusho ya kihistoria na hata kushawishi Jeshi la Ulinzi waone huo ni urithi mkubwa kwa nchi na wanatakiwa kuutunza na kuuenzi.
Pia anakumbuka mwaka 2000, Meja Jenerali Romano kutoka Afrika Kusini alifika hapo kutembelea kambi hiyo akiwa na kikosi cha Afrika Kusini na hata Septemba mwaka huu alifika Waziri aliyekuwa akishughulika na wapigania uhuru wa vita vya ukombozi.
“Bado tunashawishi watu mbalimbali hasa zilizoshiriki kwenye ukombozi wa nchi zao kutafuta namna ya kufanya ili kambi hiyo iwe na maana pana ana kuliko hivi sasa.
“Kuna historia pana sana hapa kuna madarasa na mabweni ambayo yalitumiwa na watu ambao baadaye walikuja kuwa marais tunaona kuja tu hapa haitoshi tunataka kitu kifanyike ili Kongwa ijivunie utajiri huu siku moja” anasema


Madarasa yaliyotumiwa na wapigania uhuru.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa halmashauri, katika historia ya baba wa taifa kama kuna jambo kubwa ambalo alifanya ni pamoja na kutoa kambi na ardhi itumike na nchi nyingine.
“Kambi hii iliasisiwa na Umoja wa Nchi za Afrika (OAU) na hilo likaruhusu wapigania uhuru wan chi nyingine kufika Kongwa kuchukua mafunzo ya kijeshi” anasema
Anasema Rais Jakaya Kikwete ametoa ahadi ya kujenga mnara wa kumbukumbu ambao utachukua historia za nchi zote sita za Afrika ambazo zilifika Kongwa kutafuta ukombozi wan chi zao.
Pia anataka serikali kujenga vyuo katika Wilaya hiyo ili wau wafike kujifunza na Mji huo kukua kutokana na kuwa na historia pama ya ujombozi wa Afrika.
Historia inaonesha kuna Waingereza baada ya vita walifungua shamba la karanga Kongwa lakini kutokana na kutofanya vizuri wakaamua kuanzisha shamba la mifugo ambapo sasa ni kampuni ya Ranchi ya taifa (NARCO).
Afisa Mtendaji wa kongwa Mjini, Paul Mtutui anasema kambi ya wapigania uhuru ya Kongwa aimekuwa na hostoria pana na vita ya ukombozi kutokana na nchi mbalimbali kutafuta ukombozi wan chi yao wakiwa Tanzania.
Anasema licha ya kuwa na majengo yaliyotumika kwa ajili ya wapigania uhuru hao pia kuna handaki ambalo lilitumiwa na wapigania uhuru wa Msumbuji na chama cha cha Frelimo wakiongoza na samora Machel ambaye baadaye alikuja kuwa Rais wa kwanza wan chi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1975.
Anasema handaki hilo lilikuwa likitumiwa kwa ajili ya kujificha na kufundishia wapigania uhuru.
Hata baada ya wanajeshi hao kuondoka  kambi ya Jeshi  ilikuwa ikitumia majengo hayo.
Pia Klabu ya pombe iliyokuwa ikitumia na wapigania uhuru hao sasa imebadilishwa na kuwa kituo cha afya.
“Hata Rais wa Uganda, Milton Obote alipopinduliwa na Idd Amini alikuja kujificha Kongwa” anasema
Anasema wakati huo Obote alikuwa amejificha kwenye safu ya milima ya kiboriani eneo la Mlanga ambalo ni sehemu ya kata ya Kongwa.
“Hapa kuna makazi ya zamani ya  Samora Machel na kambi hii ilipofungwa wakahamia Mazimbu Morogoro lakini hakukaa sana tangu atoke hapa nchi yake ikapata uhuru 1975” anasema
Pamoja na hayo anasema licha ya wapigania uhuru hao kuishi hapo lakini waliacha watoto kwa wenyeji.
“Walikuwa wakifika kijijini, wakawa na mahusiano na watu wa huku, walipoondoka waliacha watoto wengi tu na sasa kuna watoto wengi wa askari wa Namibia” anasema
Japo ni miaka mingi ilimepita lakini kuna watoto waliachwa na wanajeshi hao japo wengine walichukuliwa na baba zao wakati wakindoka Tanzania.
Anasema mwaka 1996 alifika Askari wa Namibia ambaye alishiriki kwenye kambi ya wapigania uhuru, Nakonkwa,  akakusanya watoto ambao baba zao ni wanajeshi wa Namibia na akaahidi kuwafuata watoto waliobaki lakini mpaka saa hajaonekana tena kurudi.
Anasema watoto waliochukuliwa wakati ule walikuwa sita wenye umri wa miaka kati ya 15 na 17.
“Wengine bado hapa kijijini mpaka sasa na wengine wana wajukuu wameshakuwa watu wazima sasa” anasema
Anasema mmoja wa watoto wa wanajeshi hao ambaye ni msichana aliyechukuliwa wakati wapigania uhuru hao kuondoka, ameamua kurudi Kongwa kutoka Namibia.
 
Nyumba aliyoishi Rais wa kwanza wa Msumbiji hayati Samora Machel iliyopo Kongwa.
Kaimu Afisa Maenseleo ya Jamii Wilaya ya Kongwa, Pascalina Duwe anasema huo ni urithi mkubwa katika vizazi vya sasa na vijavyo na kuna kila sababu kwa watanzania kutembelea kambi hiyo ili kujifunza namna Tanzania ilivyoshiriki kwenye vita vya ukombozi wa nchi nyingine.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Alfred Msovella anasema, historia ya Mji huo ni pana ikihusishwa na uwepo wa ukoloni na uchumi wa kikoloni ambao unajionesha kupitia mradi wa karanga ambapo baada ya mradi huo kushindwa wakoloni wakawa na wazo la kuanzisha ranchi mwaka 1948 baada ya vita ya pili ya dunia.
Anasema hapo kukawa na ujenzi wa reli na sura ya kuuza mazao na uwepo uchumi wa kikoloni.
Anasema historia ya ukombozi kusini mwa Afrika ilifanya mataifa ya Afrika  yapate uhuru  wake kwa kutumia miundombinu waliyoaha wakoloni kuwa mahali pa kufundishia wapigania uhuru na hata Marais Samora Machel na Sam Nujoma.
“Kwa kutumia miundombinu iliyoachwa na wakoloni wakaona watumie kuweka kambi ya wapigania uhuru jambo zuri hata Marais kama Samora na Nujoma waliwahi kuishi Kongwa” anasema
Hata nyumba aliyokaa Samora ilifanana na zile za Shirika la Reli kwani inavyoonekana ni mengo ambao  shirika la reli limekuwa likitumia katika ujebzi wa nyumba zake1980 zimambwe, 1990 namibia
Mkuu huyo wa Wilaya anasema baada ya Nchi zote kupata uhuru likafuata suala la kukomesha ubaguzi wa rangi hasa nchi Afrika Kusini.
Pia anasema utajiri mwingine wa kihistoria uliopo kongwa ulikuwa ni uenezaji wa dini hasa Anglikana kulichochewa na kuwepo kwa Chuo cha Theolojia cha Mlanga ambapo maaskofu wengi wa zamani walipata mafunzo hapo na viongozi wengi wa kanisa wamepitia hapo.
Anasemma ukitazaa matukio yote hayo, Chuo cha Interejensia,, mahandaki, sehemu aliyoishi Samora na Sam Nujoma na ukombozi wenyewe ni fursa muhimu  utalii wa kiutamaduni unaoweza kufanyika katika eneo hilo.
Anasea hata ukifika Narco Konga kuna behewa kubwa la treni ambalo lina historia ya wakoloni ni fursa nzuri ya watu kutembelea kujifunza.
Pia hata watu waliopita Mlanga wana historia kubwa ya kujifunza, kuna shule za wakoloni, hospitali ya kuaminika vyote ni fursa nzuri za kutembelea na kujifunza.
“Waziri aliyepigania vita vya uhuru wa Afrika Kusini alikuja hapa na wenzetu huko kwao fursa hii zinatumika kama sehemu ya utalii kama chumba alicholala Nelson Mandelea alipokuwa gerezani sasa ni utalii mzuri sana watu wanatembelea na sisi tunatakiwa kufanya hayo” anasema
Pia anasema Samora aliishi sana Kongwa na kuna aminika kuwa kwenye handaki kulikuwa na njia ambayo ilikuwa ikipita chini kwa chini hadi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi.
“Kitendo cha kufanya eneo lile kuwa shule kutafuta ile historia iliyopo tungefanikiwa kila kitu kilichopo kungekuwa na sehemu kubwa ya utalii kwani hata watu waliokaa pale wana ushuhuda mkubwa zaidi” anasema
Msovella anasema kuna wazungu waliishi Kongwa miaka ya nyuma lakini walipofika Kongwa wameshangaa  kwa nini Kongwa inakuwa kame.
Anasema miaka ya nyuma Kongwa ilikuwa na maji mengi lakini sasa imekuwa kame kutokana na uharibifu wa mazingira.

Friday, December 5, 2014

St John wajipanga kuondoa migogoro



KUFUATIA mgomo wa walimu na wanafunzi katika Chuo Kikuu cha St John
cha Mjini hapa Mkuu mpya wa Chuo hicho Profesa Emmanuel Mbennah
amesema  wamejipanga  kuhakikisha changamoto zinazokikabili chuo hicho
 zinashughulikiwa  katika muda mfupi ujao.
Alisema hayo jana wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi
kufuatia mgomo wa walimu na wanafunzi unaoendelea chuoni hapo ambapo
walimu wamekuwa wakidai kuongezewa maslahi na wanafunzi wakitaka
kutengenezewa mazingira mazuri ya kusomea na kusajili wa kwa kozi
NACTE.
Profesa Mbennah alisema muda mfupi ujao chuo hicho kitakuwa mahali
bora na pazuri pa kutolea taaluma kwa wanafunzi na wahadhiri
mbalimbali kufanyia kazi, hivyo kuomba wapewe muda kuyashughulikia.
Alisema, uongozi uliopo ni sikivu na umepokea changamoto zote
zinazokikabili chuo hicho hususani kutoka kwa wanafunzi na wahadhiri
wote na upo tayari kuzichambua na kuzishughulikia mapema iwezekanavyo,
ili chuo hicho  kiwe mahali bora na pazuri pa kusoma na kwa wahadhiri
kufanyia kazi.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na baadhi ya kozi
kutokusajiliwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NACTE), uchache wa
wahadhiri mbalimbali chuoni hapo na vitendea kazi vya kutosha
kufundishia ili chuo kiweze kutoa taaluma nzuri na bora.
Alisema, kulingana na mahitaji ya viwango vya kozi za kilimo na
maabara ya tiba za magonjwa ya binadamu katika kozi za ufundishaji
ngazi za cheti na astashahada, NACTE walitoa sharti la kukamilisha
chumba cha mafunzo kwa vitendo ili chuo kiweze kupata usajili wa kozi
hizo mbili.
Alisema tayari chumba hicho cha mafunzo kwa vitendo kimekamilika, na
jana alikikagua na kuridhika na mahitaji kama yalivyoainishwa na
NACTE, na tayari ameshauandikia  uongozi wa NACTE kuja chuo hapo ili
kukagua na kutoa usajili huo.
Pia katika kutatua upungufu wa wahadhiri chuoni hapo, chuo kinatarajia
kuajiri waaimu wapya Desemba mwaka huu na kwa sasa kinaendelea kutumia
baadhi ya wahadhiri kutoka vyuo vingine vya elimu ya juu vilivyopo
hapa Dodoma, kusaidiana na wahadhiri waliopo chuoni hapo.
Alisema walichokubaliana na uongozi wa serikali ya wanafunzi (SOSJUT)
kwa kushirikiana na uongozi wa Kaimu Mkuu wa Chuo Taaluma washirikiane
kutayarisha andiko maalumu litakalotumwa kwa baraza la chuolikielezea
mapungufu ya mfumo wa sasa yaliyopo na jinsi wanafunzi wanavyoathirika
na viwango hivyo vya zamani vya utoaji wa alama za ufaulu, kisha
yatajadiliwa na baraza la seneti na kuyatolea majibu.
Suala lingine la wanafunzi ni kuhusu kutosajiliwa kwa baadhi ya kozi
za fani ya kilimo na maabara za tiba. Mkuu huyo alisema kwamba, jambo
hili limeshakamilika  na NACTE muda wowote watafika kwa ukaguzi wa
maagizo waliyotoa kwa chuo ili yatekelezwe na kisha kutoa usajili.
Pia alitoa wito kwa wanafunzi wote katika fani hizi wasiwe na mashaka,
kwani muda mfupi ujao watakamilisha mafunzo yao na kupatiwa vyeti
vyao.
Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Daniel Damian alisema ni
muda mrefu palikuwa na mazungumzo kati ya uongozi wa chuo na serikali
ya wanafunzi kuhusu masuala mbalimbali na uongozi wa wanafunzi
uliwasilisha rasmi changamoto zao kwa uongozi wa chuo na kuahidiwa
kujibiwa.

Asiye na choo hupoteza siku 2 kwa mwaka kutafuta pa kujisadia

TANZANIA inapoteza jumla ya shilingi bilioni 301 kila mwaka kama gharama ya kukabiliana na madhara ya uchafu wa mazingira.Hayo yalisemwa jana na Meneja wa Mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA), Kornel Kema wakati akizungumza kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya usafi wa mazngira iliyofanyika Dodoma.
Huku akinukuu ripoti ya Benki ya Dunia ya Programu ya Usafi wa Maji na Mazingira iitwayo ‘Madhara ya Kiuchumi yatokanayo na hali duni ya usafi wa mazingira afrika’, Bw. Kema alisema kuwa fedha hizi ni nyingi na kwamba zingeweza kuokolewa kama usafi wa mazingira ungeboreshwa nchini.
Kwa mujbu wa ripoti hiyo, jumla ya Watanzania  milioni 26 wanatumia vyoo duni na pia zaidi ya watu milioni tano hawana choo na kwamba wanajisadia haja ndogo na kubwa kwenye maeneo ya wazi.
Pia inaonesha kuwa mtu mmoja asiye na choo bora hupoteza muda wa siku mbili na nusu kwa mwaka katika kutaafuta eneo la kujisadia katika maeneo ya wazi ili watu wengine wasimuone.  
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na mradi wa UMATA yalifunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa.
Kwa mujibu wa Mkwasa alisema pamoja na kwamba Dodoma ina matatizo makubwa ya upatikanaji wa maji lakini hilo lisiwe kisingizio cha kutotiliaa maanani usafi wa mazingira.

“Hatuwezi kuacha wananchi wasijali usafi kkwa vile kuna tatizo la maji , usafi wa mazingira si kuoga tu ni usafi wa jumla katika kaya na hata kuhakikisha kuna choo bora” alisema
Mradi huo unafadhiliwa na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usafi wa Mazingira (GSF) na kutekelezwa na Shirika la Plan International katika wilaya za Bahi, Chamwino na Kongwa mkoani Dodoma.



Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali (hawapo pichani) kabla ya kuzindua rasmi mafunzo yao juu ya mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA) Kulia ni Mkurugenzi wa Mradi wa UMATA, Nyazobe Malimi na kushoto ni Meneja wMradi huo, Koronel Kema.








Afisa Afya wa Mkoa wa Dodoma, Edward Ganja, akifafanua jambo juu ya hali ya afya na usafi wa mazingira kwa mkoa wa Dodoma alipokuwa akizingumza na waandishi wa habari wanaotoka vyombo mbali mbali vya habari wanaohudhuria mafunzo juu ya mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA) .

Kulia ni Mkurugenzi wa Mradi wa UMATA, Nyazobe Malimi na kushoto ni Meneja wa Mradi huo, Koronel Kema.


Add caption

Mkazi wa mpwapwa ajifungua mtu kama chura

MKAZI wa  wa   kijiji cha  Chibwechangula –Behelo  katika Wilaya ya
Mpwapwa Mkoani Dodoma, Ruth Matonya (26)  amejifungua mtoto wa ajabu
ambaye nusu ya sura yake ilikuwa ikifanana na binadamu na nusu
ikifanana na chura.
Mtoto huyo alizaliwa Desemba 2, mwaka huu katika Kituo cha Afya cha
Mtakatifu Luka  kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana  Dayosisi ya
Mpwapwa. Ambapo alifariki dakika chache baada ya kuzaliwa.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dk. Edwin Kihura  mara
baada ya mama huyo kufika kituo hicho cha afya alikuwa na uchungu
mkali  ambao uliendelea bila kukoma na baadaye alishindwa kujifungua
kwa njia ya kawaida licha ya kuwa njia ilikuwa imefunguka.
Alisema kutokana na hali hiyo ilimazimika mama huyo kufanyiwa upasuaji
 ili kuweza kuokoa maisha yake na mtoto.
Alisema  wakati mama huyo akihudhuria kliniki walipojaribu kupima
miezi ya mwisho mama huyo  lakini mkao wa mtoto ulikuwa haupatikani,
wala mapigo  ya mtoyo yalikuwa hayapatikani lakini mtoto alikuwa
anacheza tumboni jambo ambalo lilikuwa likiwashangaza sana  waganga na
manesi kituoni hapo.
Dk. Kihura alisema mara baada ya mama huyo kufanyiwa upasuaji
waliweza kutoa mtoto wa jinsi ya kike  ambae alikuwa na  sura isiyo
eleweka na kichwa kilikuwa nusu  na sura ya binadamu na nusu ikiwa ni
sura inayofanana na chura lakini viungo vyake vyote vikiwa kamili.
Alisema zipo sababu kadha ambazo  zinazoweza kusasabisha tatizo kama
hili ambapo alisema kuwa ni  baadhi ya akina mama kukosa baadhi ya
madini mwilini na  uumbaji kuto kamilika ambao unasababishwa na sababu
za kibailojia   ambazo ni kushidwa kugawanyika kwakromozome.
Alisema tatizo hilo kitaalam linajulikana kama Anecephaly.
Pia alisema matatizo kama hayo huweza kutokea  mala chache sana katika
hospitali nyingi lakini vitendo hivi vimekuwa vikiongezeka  kwa wingi
kwa siku za hivi karibuni .
Alisema hali ya mama huyo inaendelea vizuri  na pia huyo alikuwa ni
mtoto wake wa tano.