Friday, December 5, 2014

Asiye na choo hupoteza siku 2 kwa mwaka kutafuta pa kujisadia

TANZANIA inapoteza jumla ya shilingi bilioni 301 kila mwaka kama gharama ya kukabiliana na madhara ya uchafu wa mazingira.Hayo yalisemwa jana na Meneja wa Mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA), Kornel Kema wakati akizungumza kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya usafi wa mazngira iliyofanyika Dodoma.
Huku akinukuu ripoti ya Benki ya Dunia ya Programu ya Usafi wa Maji na Mazingira iitwayo ‘Madhara ya Kiuchumi yatokanayo na hali duni ya usafi wa mazingira afrika’, Bw. Kema alisema kuwa fedha hizi ni nyingi na kwamba zingeweza kuokolewa kama usafi wa mazingira ungeboreshwa nchini.
Kwa mujbu wa ripoti hiyo, jumla ya Watanzania  milioni 26 wanatumia vyoo duni na pia zaidi ya watu milioni tano hawana choo na kwamba wanajisadia haja ndogo na kubwa kwenye maeneo ya wazi.
Pia inaonesha kuwa mtu mmoja asiye na choo bora hupoteza muda wa siku mbili na nusu kwa mwaka katika kutaafuta eneo la kujisadia katika maeneo ya wazi ili watu wengine wasimuone.  
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na mradi wa UMATA yalifunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa.
Kwa mujibu wa Mkwasa alisema pamoja na kwamba Dodoma ina matatizo makubwa ya upatikanaji wa maji lakini hilo lisiwe kisingizio cha kutotiliaa maanani usafi wa mazingira.

“Hatuwezi kuacha wananchi wasijali usafi kkwa vile kuna tatizo la maji , usafi wa mazingira si kuoga tu ni usafi wa jumla katika kaya na hata kuhakikisha kuna choo bora” alisema
Mradi huo unafadhiliwa na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usafi wa Mazingira (GSF) na kutekelezwa na Shirika la Plan International katika wilaya za Bahi, Chamwino na Kongwa mkoani Dodoma.



Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali (hawapo pichani) kabla ya kuzindua rasmi mafunzo yao juu ya mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA) Kulia ni Mkurugenzi wa Mradi wa UMATA, Nyazobe Malimi na kushoto ni Meneja wMradi huo, Koronel Kema.








Afisa Afya wa Mkoa wa Dodoma, Edward Ganja, akifafanua jambo juu ya hali ya afya na usafi wa mazingira kwa mkoa wa Dodoma alipokuwa akizingumza na waandishi wa habari wanaotoka vyombo mbali mbali vya habari wanaohudhuria mafunzo juu ya mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA) .

Kulia ni Mkurugenzi wa Mradi wa UMATA, Nyazobe Malimi na kushoto ni Meneja wa Mradi huo, Koronel Kema.


Add caption

No comments:

Post a Comment