VIJIJI 20 katika Wilayani
kondoa mkoani Dodoma vinatekeleza mradi wa kuimarisha afya na usafi wamazingira
ikiwa ni pamoja ujenzi wa vyoo bora ili kuwezesha wakazi wa maeneo husika
kuondokana na na magonjwa yanayotokana na ukosefu wa vyoo kwemye makazi yao.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii
wilayani Kondoa, John Tesha, wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
juu ya mradi wa Kuimarisha afya unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la
Uswiss kupitia mradi wa HPSS-Tuimarishe Afya.Mradi huo wa Afya na Mazingira unatekelezwa na HPSS kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya kondoa katika vijiji 20.
Tesha alisema vijiji hivyo 20 viliwezeshwa kuandaa mpango wa kuboresha afya kwa njia shirikishi, pia jamii ilishiriki katika mchakato wa uchefushaji juu ya usafi wa mazingira ili kuweza kubadili tabia za jamii.
Pia kubainisha mahitaji ya vifaa mbalimbali kwaajili ya ujenzi wa vyoo bora.
Desemba mwaka jana mpango huo ulianza katika vijiji vitano ambapo wananchi hao walipewa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa vyoo bora, kwakutumia mabampa (Latrine Slab) ambayo sasa yanatumika kujengea.
Katika vijiji hivyo kuna vikundi 20 ambavyo pia wanachama wake wamefundishwa namna ya kutengeneza mabampa na uendeshaji wa mfuko wa usafi ambapo vimefungua akaunti wanazotumia kutunza fedha zinazotokana na mabamba wanayouza katika kila kaya kwaajili ya ujenzi wa vyoo bora.
Mradi huo wa Tuimarishe afya HPSS umesaidia vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa vyoo bora kupitia mfuko wake wa masoko na mpango wa masoko ya usafi.
Wanavikundi hao wanauza mabampa haya kwa wananchi ambayo kubwa linaunzwa kwa sh.20,000 na dogo sh.10,000 na moja ya sifa ya choo bora ni kuwa na sakafu inayo safishika
Katika hatua za awali vikundi vimetengeneza na kuuza jumla ya mabamba 403, ambayo tayari yamewezesha kuboresha vyoo ngazi ya kaya.
Pia kutokana na mradi huo kufanyika katika vijiji hivyo ambapo hakuna uwezekano wa kuwepo kwa sakafu inayosafishika wamebuni uwepo wa mabampa yanayoendana na mazingira yavijijini.
Alisema kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa wananchi katika mradi huo ambapo zaidi ya kaya 300 zimeagiza mafundi kuwatengezea mabamba.
Kutokana na kasi ya mradi huo kunauwezekano wa kuwezesha jamii nzima kufikia malengo ya kuhakikisha kaya zenye vyoo bora zinaongezeka kwa asilimia 50.
Takwimu za UNICEF/WHO (2012) zinaonyesha kuwa ni asilimia 16 tu ya Watanzania walikuwa wanajisaidia sehemu nyingine tofauti na choo, na ni asilimia 34 wanatumia vyoo bora, lakini pia ni asilimia 47 ambao wanatumia vyoo visivyo kidhi sifa za choo bora.
No comments:
Post a Comment