tamko la kulaani vikali kuhusishwa kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya
Dodoma kwa kumuomba Edward Lowasa agombee Urais katika uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akisoma tamko mbele ya Waandishi wa Habari,Rais wa Serikali
ya Wanafunzi wa Chuo cha St John, Daniel Damian alikanusha Wanafunzi
wa Vyuo Vikuu vya Dodoma kwenda kwa Edward Lowasa kumshinuikiza
agombee Urais.
Alikuwa akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Serikali za Wanafunzi wa
Vyuo Vikuu vikiwemo Madini (MRA)Chuo cha Elimu ya Biashara Tanzania
(CBE)Chuo cha Elimu ya Biashara (ASEK)Chuo cha Uuguzi Mirembe na
Kitivo cha Sayansi na Jamii cha UDOM.
Damian alisema wanapenda kukanusha vikali na kulaani kuwa wao
wanatumiwa na Wanasiasa na wakiwa kama Wasomi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma
,hawatumiwi kwa jambo lolote na Viongozi wa Vyama vya Siasa.
Alisema wao kama Viongozi wa Serikali za Wanafunzi kutoka vyuo Vikuu
vya Dodoma,wanapinga na kulaani kitendo cha watu wachache
wanatukiingiza katika Propaganda za Kisiasa.
Pia alisema wao kama wasomi ambao jamii inawategemea kama kioo
hawawezi kuandamana na kujikusanya kwenye nyumba ya kiongozi na
kumuomba ogombee urais wakati wanajua fika wao hawahusiki na uteuzi wa
wagombea ndani ya Taasisi yao.
Alisema kilichofanyika ni kuudanganya umma wa Watanzania kwa kupitia
kivuli cha Vijana wachache kutoka vyuo vya hapa Dodoma ambao walifanya
kwa sababu zao binafsi.
Alisema Mkoa wa Dodoma unavyuo visivyopungua nane na jumla ya
Wanafunzi wote wanaosoma katika Vyuo vya Dodoma ni zaidi ya wanafunzi
35,000 huku Chuo cha UDOM kikiwa na Wanafunzi wasiopungua 22,000 huku
idadi ya watu waliojikusanya ikiwa haizidi 230 wengi wakiwa ni
Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuia ya Wazazi.
Pia alisema ukiwatoa Wamachinga na Jumuia ya Wazazi waliokuwepo idadi
wa Wanafunzi waliokuwepo katika tukio hilo ni sawa asilimia 0.4 ya
Wanafunzi wote wanaosoma Vyuo vya Dodoma.
‘’Tunasikitika na pia tunashangazwa na dhambi tusiyoitenda
tunayobebeshwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma ambao kwa sasa tupo
katika msimu mpya wa masomo wenye changamoto mbalimbali, ni jambo
lililotusikitisha sana ‘’
Alisema Taifa linatakiwa lifahamu hawapo tayari kutumia Elimu zao bali
wametoka Vijijini kuja kutafuta Elimu ili iwawezeshe kulikomboa Taifa
na sio kuwatumikia wanasiasa kwa malengo yao.
Waliwaasa Wanafunzi popote Nchini makundi maali mbali ya
kijamii,Wakulima,Wafugaji,
kwamba watu wachache kuzungumza kwa niaba ya makundi yao.
No comments:
Post a Comment