JESHI la Polisi Mkoani
Dodoma, limesema limejipanga kuimarisha ulinzi
maeneo yote ya Mkoa wa
Dodoma katika kipindi chote cha sikukuu ya
pasaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACP),
David Misime alisema
katika kipindi cha pasaka Jeshi la polisi
limejipanga kuimarisha
ulinzi maeneo yote ya mkoa wa Dodoma na
watafanya doria za miguu,
pikipiki, magari na pia kutumia mbwa na
farasi.
Alisema kutokana na suala
la ulinzi na usalama ni la kila mtu na wadau
mbalimbali na
watashirikiana na vyombo vingine vya dola, manispaa
kampuni za ulinzi
binafsi, viongozi wa serikali za mitaa na vikundi
vya ulinzi shirikishi.
“Tunachoomba ni kila mtu
atambue ulinzi ni jukumu la kila moja na
unaanzia katika ngazi ya
familia tunaomba waendelee kushirikiana na
Jeshi la polisi kwa
kutupatia taarifa za wahalifu na uhalifu” alisema
Alitaka kila
mtu azingatie sheria za usalama barabarani ili kuzuia
ajali,kuepuka ulevi wa
kupindukia na sehemu za starehe wazingatie
sherehe.
No comments:
Post a Comment