Kijiji cha Kiboriani Wilaya ya Mpwapwa kwa kumiliki shamba la bangi.
Wanaoshikiliwa katika tukio hilo ni Chisemi Robert (34) na wenzake wawili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP), David Misime tukio hilo lilitokea Aprili, Mosi mwaka
huu ambapo watuhumiwa hao walikamatwa wakimiliki ekari moja na nusu
la shamba la bangi.
Hata hivyo kamanda Msime alisema tayari shamba hilo limefyekwa na
kuteketezwa kwa moto.
Katika tukio lingine kamanda Misime alisema watu wengine watano
wanashikiliwa na Jeshi hilo kutokana na makosa mbalimbali kufuatia
msako uliofanyika Aprili mosi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa
Dodoma.
Alisema Simon Mtundu (51) mkazi wa kijiji cha Kisisi Kata ya Kimagiyi
Wilaya ya Mpwapwa, alikamatwa akimiliki silaha aina ya Gobore lenye
Namba MP. 00202182 kinyume cha sheria za umiliki wa silaha.
Aidha katika Wilaya ya Chemba alikamatwa Mussa Madebe (20) mkulima wa
Kata ya Songolo Tarafa ya Goima na wenzake watatu wakiwa na misokoto
nane ya Bhangi.
Alisema watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara upelelezi
utakapokamilika na msako unaendelea.
Pia Kamanda Misime aliwashukuru wananchi wanaoshirikiana na Jeshi la
Polisi kwa kutoa taarifa hali inayopelekea kukamatwa kwa wahalifu.
![]() |
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi a Polisi (SACP) David Misime |

No comments:
Post a Comment