Wednesday, August 5, 2015

Wizi wa dawa za serikali wapungua

TATIZO la wizi wa dawa za Serikali limepungua baada ya kuanza kwa
utaratibu wa kuweka nembo kwenye vifungashio na kwenye vidonge.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja ya Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD)
kanda ya kati, John sipendi wakti akizungumza na waandishi wa habari
kwenye viwanja vya maonesho ya kilimo na mifugo yanayofanyika katika
Viwanja vya Nzuguni Mjini hapa.
Alisema awali MSD ilikuwa ikiweka nembo ya MSD katika vifungashio tu
ambapo ilikuwa ni rahisi dawa hizo kuhujumiwa na kwenda kusikistahili
lakini sasa nembo hiyo inawekwa mpaka kwenye vigonge..
“Kwa kuweka nembo hiyo ya GOT pamoja na MSD katika dawa ni hatua
ambayo imesaidia kupunguza ama kudhibiti kabisa tatizo la wizi wa dawa
za serikali.
Pia alisema mpaka sasa tayari aina 45 ya vidonge vimekwisha wekewa
nembo hiyo na wazabubi wenginr wote wanaopata zabuni za kupeleka dawa
MSD wanaelekezwa kuzingatia utaratibu huo wa kuweka nembo ya GOT na
MSD.
Alisema kwa sasa kuna udhibiti mkubwa  wa dawa za serikali kwenda
kwenye maduka binafsi tofauti na hapo awali wakati vidonge vilipokosa
nembo.
Hata hivyo alisema sheria iliyoanzisha MSD haina mamlaka ya kukamata
wenye maduka ya dawa lakini kama dawa yenye nembo ikikamatwa kwenye
duka la dawa binafsi hatua ya kisheri itachukuliw kwani ni ushahidi
tosha kuwa na dawa yenye nembo duka binafsi kwani hairuhusiwi
Pia alisema kwenye maonesho hayo kunatolewa huduma za tiba kwenye
banda la hospitali ya mkoa wa Dodoma ambapo wagonjwa baada ya
kuandikiwa dawa huenda kuchukua kwenye banda la MSD bila malipo
yoyote.
Alisema pamoja na hangamoto zoye ambazo MSD inakabiliana nazo bado
wameendelea kuboresha huduma zao kwa kuhakikisha madawa yanapatikana
kwa wakati
Alisema changamoto nyingine ni raslimali fedha na serikali bado
inaendelea kulipa deni lake japo haijakamilisha malipo yote
yanayodawa.
“Tunajitahidi kuhakikisha dawa zinafika kwa wakati ili kuondoa
changamoto za ukosefu wa dawa kwenye hospitali” alisema
Kwa upande wake,Afisa huduma kwa Wateja kutoka MSD, makao makuu, Idd
Abeid alisema aliwataka wakazi wa Dodoma kufika kutemnelea banda lao
na kupata huduma ya matibabu n dawa bila malipo.
Afisa Viwango na Udhibiti wa Ubora kutoka MSD makao makuu Betia Kaema
alisema mwamko wa wananchi kujitokeza kupata huduma za matibabu kwenye
banda lao ni mkubwa.

No comments:

Post a Comment