WILAYA
ya Mpwapwa iko katika hatari ya kugeuka jangwa kutokana na wananchi kukosa mbinu
za kilimo chenye kuhifadhi mazingira.
Kauli
hiyo imetolewa na maofisa wa Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS), Msanga Mabusi na Paskali Mpemba wakati
wakizungumza katika maohojiano maalumu.
Maofisa
hao wakizungumza kwa pamoja wamesema kwamba kukosekana kwa wataalamu wa kutosha
wa ugani kushawishi kilimo chenye tija na maslahi kwa mazingira kumefanya
wakulima kukata miti hovyo.
Walisema
ni jukumu la wananchi kuona namna bora ya kufanya kilimo kwa kuwa wanayahitaji
maizngira hayo ili kuwa na maisha nendelevu katika kilimo na ustawi wa jamii husika.
Mabusi
amesema kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa mazingira katika
wilaya ya Mpwapwa kunakotokana na wananchi wananchi kukosa elimu ya mbinu bora za kilimo na kutokuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.
wilaya ya Mpwapwa kunakotokana na wananchi wananchi kukosa elimu ya mbinu bora za kilimo na kutokuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Alisema
wananchi wamekuwa wakikata miti hovyo kwa ajili ya kuandaa mashamba mapya na
hivyo kutishia wilaya hiyo kugeuka jangwa kutokana na kilimo cha kuhamahama
wakitafuta maeneo yenye rutuba.
Aidha
amesema pamoja na jitihada za serikali na kuwapo kwa sheria
ya misitu namba 14 ya mwaka 2002 bado tatizo la uharibifu wa
misitu limekuwa ni kubwa na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha ya binadamu pamoja na wanyama .
ya misitu namba 14 ya mwaka 2002 bado tatizo la uharibifu wa
misitu limekuwa ni kubwa na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha ya binadamu pamoja na wanyama .
Kwa upande wake Paskal Mpemba alisema kuwa kama viongozi kuanzia
ngazi ya vitongoji ,vijiji na kata na idara tofauti hawataunganisha nguvu kulikabili uharibifu wa mazingira basi madhara yake yatakuwa makubwa na kugusa jamii nzima na kuifanya Mpwapwa kuendelea kuwa duni.
Uchunguzi
wa gazeti hili umebaini kwamba kila kijiji kina kamati ya mazingira, lakini
badala ya kukabiliana na waharibifu , nyingi ya kamati hizo zinafumbia macho
kinachoendelea kutokea cha uharibifu wa mazingira kwa kukatwa hovyo kwa miti.
No comments:
Post a Comment