Wednesday, August 5, 2015

Watia nia ubunge walalamikia mchakato

WATIA nia saba waliokuwa wakiwania kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi
(CCM) kuwania Ubunge jimbo la Dodoma Mjini wamelamikia mchakato mzima
wa kura za maoni kwa madai kuwa ulitawaliwa na  vitendo vya rushwa na
kutishia kutosaini matokeo.
Wakizungumza jana baada ya kuwasilisha  malalamiko yao dhidi ya Antony
Mavunde na haidary Gulamali na Mkurugenzi wa Uchaguzi kupinga
kutangazwa kwa kura za maoni Wilaya ya Dodoma Mjini walisema hawako
tayari kumuunga mkono mgombea aliyeshinda kwenye mhakati huo, Antony
Mavunde.
Mbunge wa Dodoma Mjini anayemaliza muda wake, David Malole alisema
vitendo vya rushwa viligubika uchaguzi huo huku watu walikuwa kwenye
foleni kupiga kura walikuwa wakigawiwa fedha ili wampigie kura
Mavunde.
Pia alisema katika kata ya Kilimani wapiga kura walioorodheshwa
walikuwa ni 2,700 lakini waliopiga kura walikuwa ni 5,000 jambo ambalo
linaleta mashaka makubwa.
Malole alisema hatakuwa tayari kumuunga mkono mgombea huyo.
Katika barua iliyowasilishwa jana wanaopinga matokeo hayo ni pamoja na
David Malole, Mussa Luhamo, Mohamed Mgoli,Antony Kanyama, Robert
Mtyani, Steven Masangia  na  Emmanuel Kamara, wakizungumza na
waandishi wa habari jana walisema hata  hata zoezi la kujinadi
lilikabiliwa na changamoto nyingi ambazo zilifanya zoezi la kura za
maoni kugubikwa na vitendo vya rushwa pia nafasi ya kujinadi kutolewa
kwa upendeleo.
Pia walilalamikia  kitendo cha mkurugenzi wa uchaguzi kutumia gari la
mgombea, mkurugenzi kushiriki kwa dhati kuharibu kampeni.
Aidha walisema hata ujumlishaji wa kura haukufanyika mbele yamawakala
wa wagombea.
“Mkurugenzi wa uchaguzi bila kuhusisha mawakala wa wagombea yeye na
katibu wa wazazi na bila taarifa kwa wagombea walihesabu kura na kutoa
matokeo ya mwisho  jambo ambalo linatia wasiwasi kwa kuwa
walishalalamikiwa na wagombea tangu awali” alisema
Pia walisema kinachowatia mashaka zaidi na Antony Mavunde kabla ya
Mkurugenzi kutangaza matokeo aliyafahamu matokeo  hayo na kuyatangaza
katika vyombo mbalimbali.
Pia walilalakimia kitendo cha Mavunde na Gulamali kuzungukia vituo vya
Chang’ombe juu na kuingia ndani.
“Tunaomba matokeo haya ya uhaguzi yabatilishwe na kurudiwa chini ya
usimamizi wa hali ya juu kwa kusimamiwa na vyombo vya dola ili haki
iweze kupatikana” ilisema sehemu ya barua hiyo ya malalamiko
iliyowasilishwa kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma Mjini.

No comments:

Post a Comment