Saturday, August 8, 2015

Sophia Simba: Sihami CCM ng'o

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Taifa  (UWT)
Sophia Simba amesema hana mpango wa kuihama CCM.
Akizungumza na waandishi jana kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa
Baraza la UWT Taifa,Simba alisema ,maneno kuwa ana mpango wa kukihama
chama hayana ukweli wowote na yeye bado ni mwanachama wa chama hicho
na hana mpango wa kuhama.
"Kama mnavyofahamu..,mimi ni Mwenyekiyi  wa UWT Taifa..,sina mpango
wowote wa kuhama chama ...,sijafikiria na wala sijawaza kuhama CCM”
alisema
Alisema kuna minong’ono mingi ambayo haina ukweli wowote.

"Ile minong'ono mliyoisika haina ukweli wowote...,kuna wazushi wana
yao wangependa pengine iwe hivyo kwa sababu mimi mnanifahamu kwa
sababu ya CCM,ninaringa kwa sababu nipo ndani ya CCM ..,sina pengine
pa kwenda...,CCM imenilea...,imenikuza ..,nitaenda nacho mpaka mwisho
wa hatma yangu."alisema

Simba ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto,
alikuwa amevalia  dira lililoandikwa ' Baki njia kuu mchepuko  siyo
dili ' alisema kuwa,Jumuiya hiyo imejipanga kuhakikisha mgombea urais
kupitia CCM, Dk.John Magufuli anashinda katika uchaguzi mkuu ujao wa
Oktoba 25 mwaka huu.

Alisema Jumuia hiyo imejipanga kuhakikisha inampeleka Magufuli Ikulu.
"UWT tumejipanga...,kama mnavyojua sisi ni jeshi kubwa
...,tutahakikisha tunampeleka Magufuli Ikulu ...,na leo tuna kikao
kizito sana cha kuweka mikakati ya kumpeleka Magufuli Ikulu,

Alipoulizwa na wanhabari kuwa watu walimzushia kukihama  chama hicho
kwa sababu alikuwa kwenye timu ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward
Lowassa alisema,katika uchaguzi ule kila mtu alikuwa na timu yake huku
akikiri kwamba naye alikuwa kwenye timu ya Lowassa.

Alisema ule ulikuwa ni mchakato ndani ya CCM ambao tayari
umeshamalizika na makundi yote yamekwisha limebaki moja la Magufuli
ambalo ni kundi la CCM .

Simba alisema kila mtu aliwaza kwa sababu zake kwamba atakihama chama .
“Hayo ni mawazo tu...,huwezi kumzuia mtu kuwaza...,lakini mimi
niliingia CCM kwa sababu zangu na sina sababu yoyote ya kuondoka CCM,
maana ndicho kimenilea na kunikuza” alisema Simba na kuongeza

"Kama Lowassa amehama chama ana sababu zake za msingi...,mimi sina
sababu yoyote ya kufanya hiyo...,tulikuwa na timu...,sasa tumevunja
..imebaki timu moja tu Magufuli ambayo ni kambi ya CCM."

Aidha alisema hakuna mpasuko wowote ndani ya CCM kutokana na kuondoka
Lowassa kwani pamoja na kuhama kwa baadi ya wanachama bado CCM ina
mamilioni ya wanachama.

Alisema ,wanaodai kuna mmomonyoko kwa kuondoka Lowassa CCM siyo kweli
huku akisema hizo ni propaganda za kisiasa lakini kimsingi hakuna
mmomonyoko wowote.

"CCM hatutishiwi nyau..,uwezo wetu ni mkubwa” alisema

Alisema kaulimbiu ya UWT ni 'wanawake jeshi kubwa Magufuli Ikulu ni lazima.'

Awali alifungua Mkutano wa baraza la UWT Taifa wa uchaguzi wa
wawakilishi wa Bunge, kwenye makundi mbalimbali Simba ,aliwataka
wajumbe watakaoshinda katika uchagzui huo kuhakikisha wanakwenda
kufanya kazi ya kuhakikisha  CCM inapata ushindi mkubwa katika
uchaguzi mkuu ujao.

Alisema kuna baadhi ya wagombea wakishinda badala ya kwenda kufanya
kazi wanakwenda kutafuta nguo za kwenda kutambishia Bungeni.

"Wale watakaoshinda waende kufanya kazi,wengine wakishinda
wanakimbilia Ulaya kutafuta nguo za kwenda kutesea  Bungeni” alisema
Alisema kamati ya maadili itakuwa inawaangalia kwani baada ya zoezi
hilo hakuna kulala mpaka kieleweke.
Pia aliwataka wajumbe kuchagua viongozi  watakaokwenda kuwawakilisha
bungeni badala  ya kuchagua watu ambao baadaye watawalalamikia.

Aliwataka kuchagua majembe ya kwenda kufanya kazi.
“Tunataka watu wanaojiamini na watakaokwenda  kuzungumza Bungeni” alisema

Pia aliwataka watakaoshindwa kutulia ndani ya chama kwani kuna nafsi
nyingine nyingi na  siyo kuhama chama.
Add caption

No comments:

Post a Comment