MKUU wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa amewataka wadau,wawakilishi wa
wananchi kushiriki kutoa maoni yao juu ya mradi ujenzi wa bwawa la
Farkwa ili kusiwepo na mamalmiko siku za usoni.
Alisema hayo jana wakati akifungua kikao cha wadau cha kujadili
taarifa ya tathimini ya athari kwa mazingira na jamii ya mradi wa
bwawa la Farkwa
Pia alisema tangu kuanza kwa mradi huo wadau, wawakilishi wa wananchi
wamekuwa wakishirikishwa ili kusiwepo lawama kwa siku zijazo.
Alisema mradi wa bwawa utaongeza upatikanaji wa maji katika Jiji la
Dodoma, vijiji litakapopita bomba kuu pamoja na Wilaya ya Chemba na
maeneo mengine yanayoguswa na mradi.
Pia mradi huo utanufaisha wananchi wa Wilaya ya Bahi katika skimu za
umwagiliaji, kukamilika kwa mradi huo kutaleta chahu ya maendeleo ya
kijamii na kiuchumi kwa Jiji la Dodoma na maeneo mengine.
Alisema tathimini itasaidia kuonesha ni kwa kiwango gani mradi huo
unawez kuathiri au kutoathiri shughuli zingine za kiuchumi na kijamii.
Galawa alisema takwimu za tafiti za wanasayansi zinaonekana maji
yanayotumika kwa ajili ya shughuli za kibinadamu na viumbe wengine
yanaendelea kupungua.
Kwa upande wake, katibu Mkuu Wizara ya Maji,Mbogo Futakamba alisema ni
utaratibu uliopo katika kushirikisha wadau katika hatua mbalimbali ili
kila moja kufahamu hatua iliyofikiwa ili kuweza kuchukua hatua muhimu
kwa ajili ya wananchi.
“Suala la upatikanaji maji imekuwa changamoto dunia nzima kutokana na
mabadiliko ya tabia nchi na kumekuwa na vipindi virefu vya ukame na
hata mafuriko” alisema.
Alisema serikali imeweka kipaumbele kwenye masuala ya maji
Mkurugenzi wa raslimali za maji Nchini, Hamza Sadiki alisema ujenzi wa
bwawa hilo umuhimu mkubwa, kwani sasa hata chanzo cha maji cha
makutupora kimeanza kulemewa.
Alisema kuna mambo ya kuhoji baada ya ujenzi wa bwawa kutakuwa na
athari gani za kimazingira.
Alisema kazi ya usanifu inafanywa na makamapuni mbalimbali ya nje
ambayo yamesajiliwa nchini.
Alisema kazi ya tathimini ya mazingira ya kijamii inaendelea sambamba
na kazi ya usanifu.
Baada ya kumalizika kwa tathimini na maoni kupatikana mshauri
mwelekezi atamalizia kazi aliyopewa.
Alisema ujenzi wa bwawa unatarajia kuanza mwishoni mwa mwaka huu wa fedha
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Francis Mwonga alisema kumekuwa na upotoshaji
kuhusu ujenzi wa bwawa hilo, ambapo katika wilaya ya Bahi watu
wamekuwa wakitegemea maji hayo kwa ajili ya kilimo, kunyewshea mifugo
na kuna taasisi zinatumia nafasi hiyo kupotosha wananchi kuwa iwapo
bwawa litajengwa watakosa maji kwa ajili ya matumizi yao.
No comments:
Post a Comment