KAMPUNI ya simu
ya Vodacom imekabidhi kompyuta tatu na mtambo wa kuunganisha
kompyuta kwa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 5.3
Mwakilishi wa kampuni hiyo, Salum Mzee amesema kompyuta hizo zimetolewa ili kutimiza ahadi
waliyoitoa na kutaka vifaa hivyo kutumika kwa ajili ya kusaidia kazi za
uandishi wa habari Mkoani Dodoma
Amesema Vodacom inatambua mchango wa waandishi
wa habari kwa kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikifikia jamii ambao ndiyo
walengwa.
Mwakilishi huyo wa Vodacom amesema mwaka jana walipitisha mpango maalum wa
kusaidia vyama vya waandishi wa habari ambapo Sh. Milioni 40 zilitengwa na hadi sasa mikoa iliyofaidika ni
pamoja na Tanga, Kagera, Iringa na Dodoma
Pia ameitaka CPC kuhakikisha vifaa
hivyo vinatumika kwa shughuli iliyokusudiwa ya kuanzia mradi wa internet.Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatma Ally alitaka vifaa hivyo vitunzwe vizuri ili viweze kutumika kwa muda mrefu.
![]() |
Mwakilishi wa Kampuni ya simu ya Vodacom, Salum Mzee akizungumza wakati wa kukabidhi kpmpyuta tatu kwa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC)
|


No comments:
Post a Comment