Mwimbaji wa nyimbo za injili, Mary Sinkala ni miongoni mwa waimbaji watakaoshiriki Tamasha la Krismas litakalofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, Desemba 25 mwaka huu.
Thursday, December 12, 2013
Waimbaji kutoka Kenya, Somalia ndani ya tamasha la X mas
WAIMBAJI wa nyimbo za Injili kutoka ndani na nje ya Nchi wanatarajia kutubuiza katika Tamasha la kusifu la Shangwe za Xmas linalotarajia kufanyika desemba 25, mwaka huu
Miongoni mwa wasanii kutoka nje ya nchi ni Tumsifu Rufutu kutoka Kenya .
Msanii huyo anatamba na wimbo la Mwambie Farao, pi msanii mwingine ametajwa kuwa ni Mary Sinkala mwenye asili ya Somalia.
Tamasha hilo litafanyika kwenye Uwanja wa jamhuri ambapo mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma wanatarajiwa kuhudhuria.
Mary anatamba na wimbo wake wa wa Mkumbuke Muumba wako. Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni Beatrice William kutoka Jijini Dar es saalam aliyeanzia Bongo Star Search na kuamua kuokoka na kujikita kwenye nyimbo za injili huku akitamba na wimbo wa akina Delila wapo.
Waimbaji wengine ni pamoja na Sospeter Jonas, Mzungu mzee wa Mshumaa
Waimbaji hao wameshawataka wakazi wote wa mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kwani wamepanga kutoa burudani nzuri yenye lengo la kumtukuza na kumsifu Mungu na pia watawafundisha namna ya kumkumbuka muumba wao na
jinsi ya kuelekea kaanani.
Kiingilio katika tamasha hilo ni Sh 2,000 kwa wakubwa na Sh 1000 kwa watoto lengo likiwa ni kuwezesha watu wengi kumudu na kuhdhuria katika tamasha hilo.
Tamasha hilo litawaunganisha waimbaji toka ndani ya nchi hasa
wa mikoa ya DSM na Dodoma itakayobebwa na waimbaji toka makanisa mbalimbali na wachuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa mujibu wa mmoja wa waandaji wa tamasha hilo ambaye ni msemaji wa kampuni ya Liberty Promotion ,John Banda lengo la tamasha hilo ni pamoja na kuwachangia watoto
yatima, wasiojiweza na wale walio katika mazingira magumu.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Mary Sinkala ni miongoni mwa waimbaji watakaoshiriki Tamasha la Krismas litakalofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, Desemba 25 mwaka huu.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Mary Sinkala ni miongoni mwa waimbaji watakaoshiriki Tamasha la Krismas litakalofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, Desemba 25 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment