WAJASIRIAMALI Mkoani Dodoma wamepatiwa mafunzo ya kujengewa uelewa wa mchakato mzima wa uwepo wa mtengamano wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Akifungua mafunzo hayo kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo Mkoa wa Dodoma (TCCIA),Peter Ollomi alisema Tanzania ina wizara mahusus ya kusimamia na kuratibu uendelezaji wa mtangamano wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Alisema dira ya wizara ni kuwa na Jumuia iliyoshamiri na inayowezesha Tanzania kunufaika kiuchumi, kijamii na kisiasa na kuwa dhamira ya kuhakikisha Tanzania inashiriki kwa ufanisi katika kujenga jumuia ya Afrika mashariki iliyoshamiri na maslahi ya taifa yakizingatia vipaumbele vya Tanzania katika jumuia hiyo.
Alivitaja vipengele hivyo kuwa ni kilimo na usalama wa chakula, viwanda, miundombinu kiuchumi, utalii na nishati.
Aliwataka wajasiriamali kutumia fursa zilizopo katika mkoa ili kuweza kujiiunua kiuchumi.

kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo Mkoa wa Dodoma (TCCIA),Peter Ollomi akizungumza wakati wa mkutano huo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wajasiriamali walengwa wa mtengamano wa Afrika Mashariki.

Washiriki wa mafunzo kwa wajasiriamali walengwa wa mtengamano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment