WAZIRI wa
Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) ambalo linatoa fao la matibabu
kushirikiana na watoa huduma kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora za
matibabu.
Alitoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati akifungua mkutano
wa sita wa watoa huduma ya matibabu kwa mpango wa fao la matibabu.
Waziri Kabaka aliwakumbusha watoa huduma
kushirikiana na NSSF katika kuboresha na kuimarisha mafao hayo kwa kutoa huduma
nzuri na bora za matibabu kwa wanachama wa NSSF pamoja na wategemezi wao
walioainishwa na kanuni za fao la matibabu.
Alisema wajibu mwingine kwa watoa huduma ni
kuhakikisha wanawaelewesha wanachama wa SHIB kuhusu stahili zao na mipaka yao
ya matibabu chini ya mpango wa SHIB bila kuwachanganya au kuwalipisha gharama
mara mbili.
Kabaka alisema katika kipindi hiki fao la matibabu limepitia changamoto mbalimbali ikiwemo
viwango vya huduma zisizoridhisha kwa
baadhi ya watoa huduma, wanachama kutopewa huduma stahili wanapofika kwa watoa
huduma kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa dawa.
Pia ufahamu mdogo wa wanachama juu ya stahili yao ya
kupta matibabu bila malipo kutoka NSSF, baadhi ya wanachama kusita
kujiandikisha kwa dhana kwamba watakatwa mafao yao wakati wnapofika umri wa
kustaafu wakati si kweli pamoja na watoa huduma kutowasilisha NSSF takwimu sahihi
mafao ya matibabu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani
Dau alisema pamoja na mafanikio wanashuhudia baadhi ya watoa huduma yaani
hospitali wanatoa huduma chini ya kiwango.
Alisema mpango huo wa fao la matibabu unafanyiwa
maboresho ya kimfumo ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma.
Dk.Dau alisema NSSF kwa kushirikiana na na taasisi ya PharmAccess International
imeanza utaratibu wa kufanya tathimini
kwa watoa huduma .
No comments:
Post a Comment