Thursday, November 14, 2013

biashara ya miti shamiri manispaa ya Dodoma


Mkazi wa Dodoma, akichagua miti ya matunda kutoka kwa muuzaji kama
alivyokuwa jana na kamera yetu
BIASHARA ya miche ya miti imeanza kushamiri katika Manispaa ya Dodona kutokana na msimu wa mvua kukaribia.
Mwandishi wetu alishuhudia  baadhi ya wauzaji wa miche ya miti mbalimbali ikiwemo ya kivuli, matunda na maua.
 


Mmoja wa wafanyabiashara hao  Ayub Chitete alisema amekuwa akiuza mti moja wa matunda ana ya mchungwa kwa Sh. 2,000 na mche wa muembe kwa Sh. 3,000
Alisema miche ya maua na ile ya kivuli huuzwa kwa bei ya maelewano na mteja.
Alisema  biashara hiyo imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo wateja kuomba kupunguziwa bei licha ya kuwa kutunza miche hiyo kumekuwa ni harama kubwa.
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Dodoma wakiongea na mwandishi walisema ni muhimu kama wananchi watapata hamasa ya kununua miche ya miti ili kuipanda kama  sehemu ya kuboresha mazingira.


No comments:

Post a Comment