SERIKALI imesema kuanzia sasa itawaondoa kwenye orodha
ya ujenzi wa miradi ya maji Nchini makandarasi wote wanaochelewesha na wanaojenga miradi hiyo chini ya kiwango.
Naibu Waziri wa Maji Dk. Binilith Mahenge alisema hayo juzi Mjinihapa wakati wa ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi ya majikatika Manispaa ya Dodoma.

Alisema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kutekelezaujenzi wa miradi hiyo lakini kuna baadhi ya makandarasi wanaozembea hali inayofanya miradi mingi ichelewe kukamilika huku mingine
ikijengwa chini ya kiwango.
Akiwa katika mradi wa maji wa Ng’ong’ona ,alizungukwa na wananchi waliotaka mkandarasi wa mradi huo afukuzwe kwkushindwa kazi na wamekuwa wakipata tabu kutokana na kununua ndoo moja ya maji kati ya
Sh. 300 hadi Sh. 700.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Robert Kitimbo alisema hadi Desemba 28 mwaka huu, kama mkandarasi huyo atakuwa hajamilisha mradi huo atafukuzwa na kisha kupelekwa mahakamani.
“Mtu mwenye uwezo anafanya kazi na kisha analipwa fedha hii Kampuni ya
Dabenco Enterprises Limited sitaki hata kuisikia inaomba tena kazi ya
ujenzi wa miradi ya maji” alisema Kitimbo
Alipohojiwa kwa nini ameshindwa kumaliza mradi huo kwa wakati, Meneja
Mradi wa Kampuni ya Dabengo Emmanuel Wambura, alisema alikuwa
akisubiri fedha kutoka Manispaa ndipo aendelee na kazi ya kuchimba
mitaro iliyobaki na kuweka mabomba.
Alisema baada ya Manispaa ya Dodoma kuahidi kumlipa Sh. Milioni 51
atahakikisha anakamilisha mradi huo Desemba 28 kama alivyoamriwa.
Hata hivyo Naibu Waziri alisema iwapo mradi huo hautakamilika Desemba
28, mwaka huu Mkandarasi huyo ataondolewa kwenye orodha ya ujenzi wa
miradi ya maji Nchini.
Mradi mwingine wa maji aliotembelea ni katika Kijiji cha Ntyuka ambapo
mkandarasi wake ni kampuni hiyo ya Dabenco .
Kwa mujibu wa Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Wambura mradi huo ulianza
kutekelezwa Mei mwaka huu mpaka sasa kilichofanyika ni kuchimbwa kwa
msingi wa tenki la kuhifadhia maji na mradi huo unasuasua kutokana na
fedha kutopatikana kwa wakati.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Manispaa Dodoma alisema mkandarasi hiyo
alipewa fedha za kianzio milioni 50 lakini hata alipopeleka cheti
(certificate) kazi ya milioni 50 iliyofanyika haikuonekana.
Alisema ni maagizo ya serikali kulipa fedha pale ambapo kazi inaonekana.
“Ninachokiona hapa ni ufuatiliaji dhaifu kwa upande wa manispaa kwani
Milioni 50 zimetumika na hakuna kilichofanyika na mtu anadai fedha
nyingine” alisema naibu Waziri.
Aliagiza kuitwa kwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo
ambaye anaishi Jijini Dares salaam kufika Dodoma kwa ajili ya kikao cha pamoja.
“Naagiza Mkurugenzi huyo aje Dodoma siku ya Jumamosi naona meneja wake
hakuna anachofahamu kama hawezi kazi tutamwambia basi kwani
makandarasi ni wengi” alisema
Katika taarifa yake Kitimbo alisema mradi ya Ng’ong’ona
utakapokamilika utagharimu jumla ya Sh. Milioni 488.3 ambapo mpaka
sasa jumla ya Sh. Milioni 137.9 zimelipwa na mradi a Ntyuka utagharimu
kiasi cha Sh. 387.4 ambapo mpaka sasa jumla ya Sh. Milioni 58.1
zimelipwa.
mwisho

No comments:
Post a Comment