![]() |
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo (Wa tatu kutoka kulia) akicheza muziki na wahitimu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Dodoma mwishoni mwa wiki ambapo aliibuka mshindi |
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi,Philip Mulugo juzi aliibuka mshindi katika shindano la kucheza muziki
wa kwaito wakati wa mahafali ya 30 ya Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi
(VETA) Dodoma
Mulugo alikuwa akishindana pamoja na
wahitimu wa fani mbalimbali ambao baadaye aliwatunikia vyeti.
Mshindi wa shindano hilo alipatikana
kutokana na maoni ya wanafunzi na wazazi ambao walikuwepo katika mahafali hayo.
Akimtangaza mshindi huyo Mkuu wa Chuo
cha VETA Dodoma, Ramadhani Mataka alisema Naibu Waziri Mulugo atapata zawadi ya
kuchongewa kitanda cha futi sita kwa sita ambacho kitakuwa ni ukumbusho mzuri
kwake.
“Tutakuchongea kitanda cha futi sita
kwa sita ambacho nadhani utakipeleka jimboni mwako kiwe kwa ajili ya
kupumzikia” alisema Mataka
Jumla ya wahitimu 122 walitunukiwa
vyeti katika fani mbalimbali, ikiwemo, ujenzi, umeme na udereva
Licha ya mahafali hayo kupambwa na
burudani mbalimbali pia kulikuwa na onesho la mavazi yaliyoandaliwa na
wanafunzi wa Chuo hicho.

No comments:
Post a Comment