![]() |
| Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Dodoma, Imelda Likoko. |
(NHIF) vimekamatwa kutokana na kutumika kinyume cha utaratibu.
Hayo yalibainishwa jana na Meneja wa Bima ya Afya Mkoa wa Dodoma,
Imelda Likoko wakati wa mahojiano na waandishi wa habari.
Alisema vitambulisho hivyo vilikamatwa kufuatiwa zoezi maalum la
ukaguzi lililofanyika katika hospitali mbalimbali ikiwemo ya Mkoa wa
Dodoma,Agakhan. St. Gemma na kituo cha Afya cha Amani.
Meneja huyo alisema vitambulisho hivyo vilikuwa vya wanachama ambao
uanachama wao umekoma aidha kwa kustaafu au kwa kufariki.
“Tumewanyanyang’a vitambulisho hivyo na kuondoka navyo kwani
tulipokuwa tunakamata kadi na kuwahoji wahusika walisema wenye kadi
walistaafu au kufariki na walikuwa hawafahamu kuwa kutumia kadi hizo
ni kosa” alisema
Aidha Meneja huyo alisema kongamano la wadau waNHIF, litafanyika kesho
(Jumatatu) Mjini hapa huku dhumuni kubwa likiwa ni kutoa fursa kwa
wadau wa mfuko huo kujadiliana masuala muhimu yanayohusu Bima ya Afya
na changamoto mbalimbali zinazoukabili mfuko huo ili kupata ufumbuzi
utakaoimarisha utendaji wa mfuko ambao unahudumia Watanzania walio
wengi.
Wakati huo huo,Meneja huyo alisema wanaendelea kuhamasisha wananchi
kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa lengo la kufanya kaya
nyingi zijiunge na kuwa na uhakika wa matibabu pindi wanapougua.
Likoko alisema mfuko huo kwa kushirikiana na halmashauri za Wilaya
wamekuwa wakihamasisha wananchi ili waone faida za kujiunga na mfuko
huo.
Alisema sasa kuna udhibiti na ukaguzi wa dawa zinazopelekwa katika
hospitali na vituo vya afya ili ziweze kutumika kwa malengo
yaliyokusudiwa ili kupunguza tatizo la kukosekana kwa dawa kwenye
vituo vya kutolea huduma
Alisema mpaka kufikia Juni mwaka huu, Wilaya ya Chamwino ilikuwa
ikiongoza kwa kuandikisha wanachama kwa asilimia 17.4 ikifuatiwa na
Wilaya ya Bahi asilimia 16.5, Wilaya ya Kongwa asilimia 15.4, Wilaya
ya Mpwapwa asilimia 15.5, Manispaa ya Dodoma asilimia 4.6 ikifuatiwa
na Wilaya ya Kondoa asilimia 3.2 na Wilaya ya Chemba asilimia 2.9.

No comments:
Post a Comment