![]() |
| Nduluyaluha Wile Lusendamila akiwa katika pozi. |
.Yeye amebadilika anaenda kisasa
MFUGAJI
kutoka Kijiji cha Uhelela Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma Nduluyaluha Wile
Lusendamila amesema elimu ndogo waliyonayo wafugaji wengi inapelekea kuishi
maisha ya kimaskini licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa mifugo.
Mfugajji huyo ni kati ya wafugaji walioamua kubadilika na kuvuna mifugo yao kwa ajili ya kustawisha maisha yao.
Alianza kuvuna mifugo yake mwaka 2008 ili aweze kuishi vizuri kutokana na kuwa na mifugo mingi ambayo alikuwa haufurahii utajiri huo.
Mwaka 2004 wakati wa vuguvugu la kuhamisha wafugaji kutoka Ihefu Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya safari yake iliishia Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma ambapo aliamua kuweka maskani yake.Wakati akitoka Ihefu kwenda Bahi alikuwa na ng’ombe 1,700 na mbuzi zaidi ya 300 lakini mpaka sasa amebaki na ng’ombe 300 na maisha yake yamebadilika.
‘’Tumezaliwa kwenye mifugo hatuna elimu, naomba wafugaji wabadilike watoto wao hawasomi sababu ya utumwa wa mifugo, tuifuge sio itufuge utajiri huu unaweza kubadilishwa na kumfanya mfugaji aongeze muda wa kuishi duniani” alisema

|
Lusendamila
(kushoto aliyesimama) akiwa na familia yake (Wa pili kushoto) mwenye
kilemba ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi.
|
Kulingana na kauli yake, wafugaji wengi wamekuwa wakilala nyumba moja na mifugo jambo ambalo husababisha kuugua magonjwa mbalimbali ikiwemo kifua na hivyo kuwafanya kuwa dhaifu.
‘’Vumbi la ndani ya nyumba la kulala na mifugo ni hatari hatulogwi tunajiua wenyewe” alisema
Sasa ameweza kujenga nyumba tatu za kisasa, kusomesha watoto kwenye shule za mchepuo wa Kiingereza, kununua magari ya kutembelea na amekuwa akimiliki daladala kwa ajili ya biashara.Pia kuwasaidia ndugu zake na wazazi wake.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Alfred Msovella akimzungumzia mfugaji huyo anasema ni mfano wa kuigwa kwani ameamua kuacha kuitumikia mifugo na sasa mifugo inamtumikia yeye.
Alisema ni vizuri elimu hiyo ikatolewa kwa wafugaji katika maeneo mengine nchini ambapo ina nafasi kubwa katika uunzaji wa mazingira na kupunguza migogoro isiyo ya lazima.
‘’Alipokuwa Ihefu alionekana kama adui hafai kumbe kinachotakiwa kufanyika ni kuelimisha wafugaji” alisema
![]() |
|
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dk.Rehema Nchimbi akipanda mti nyumbani kwa mfugaji
huyo Kijiji cha Uhelela Wilaya ya Bahi.
|
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi anasema kuna haja ya kwapokea
wafugaji na kuwaelimisha kisha watulie kwani ufugaji ni moja ya malengo muhimu
katika uchumi na maendeleo katika Nchi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwasa jitihada zinaendelea za kuhamasisha wafugaji kuwa na mifugo inayoendana na uwezo wa malisho na itakayoboresha maisha ya wananchi na wafugaji.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwasa jitihada zinaendelea za kuhamasisha wafugaji kuwa na mifugo inayoendana na uwezo wa malisho na itakayoboresha maisha ya wananchi na wafugaji.
Anasema mipango hiyo ni ya muda mfupi, kati na
mrefu wa uvunaji wa mifugo.
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa akipanda mti nyumbani kwa mfugaji huyo |
Mkwasa anasema mpaka sasa wafugaji 68 wamevuna mifugo yao pia kuna mpango wa kuanzisha ushirika wa wafugaji utakao simamiwa na Benki yaCRDB.

No comments:
Post a Comment