Tuesday, November 26, 2013

RCO Nyanda afungua mkutano wa makampuni ya ulinzi


MKUU wa Upelelezi Mkoa wa Dodoma (RCO), Damas Nyanda leo amefungua mkutano wa  mwaka wa Sekta ya Ulinzi Binafsi Nchini (TSIA), katika hoteli ya Dodoma na kutafa makampuni hayo kufuata utaratibu katika utendaji kazi wake wa kila siku.
Alisema Jeshi la Polisi linatambua umuhimu wa kazi ainayofanywa na makampuni binafsi ya ulinzi.
Pia alitaka makampuni hayo kufuata utaratibu katika utendaji kazi wake na kuelewa matumizi ya programu ya ulinzi shirikishi.
Awali,Mwenyekiti wa Chama cha sekta ya ulinzi binafsi, Almas Maige alisema kwa biaba ya sekta ya ulinzi waliendelea kutafita suluhu ya matatizo makubwa ya sekta hiyio kama saa za ziada wanazolipa kwa wafanyakaiz ambazo hazilipiki kutokana na kutumia sheria ya kiraia ambayo katika majeshi haitumiki.
Pia  matatizo ya mishahara ya kijumla bila madaraja na taaluma zisizotambulika.
Pia alilitaka Jeshi la Polisi kutambua tofauti ya vyama vya kitaaluma katika sekta ya ulinzi binafsi na chama Kikuu cha sekta ya ulinzi binafsi (TSIA).
Alisema hivi karibuni kilianzishwa chama cha kitaaluma cha walinzi watu (TAMASCA) na watu wachache wala si cha Kitaifa kwa maana ya kusimamia taaluma zote za sekta ya ulinzi binafsi.
Maige alisema Jeshi la Polisi kupitia  baadhi ya maofisa ambao hawakufahamu tafsiri na uwakilishi wa chama hichjo katika sekta ya ulinzi binafsi wameanza au wamekuwa wakiwasiliana na viongozi wa sekta ya ulinzi binafsi kwa watu ambao hawana uwakilishi wa kisekta, uwezo wala  weledi wa sekta ya ulinzi binafsi.



No comments:

Post a Comment