MENEJA wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania, (TRA) Mkoa wa Dodoma , Thadey Kaliza amesema wanakusudia kukusanya
kiasi cha Sh. Bilioni 37 katika mwaka wa fedha wa Julai 2013 hadi Juni
2014 .
Alisema
hayo juzi
katika mkutano wake na waandishi wa habari juu ya Wiki ya Mlipa Kodi na
kuwataka wafanyabiashara kuona fahari kulioa kodi kwa ajili ya maendeleo
ya taifa.
Alisema katika
mwaka huu wa fedha serikali imewapangia mkoa huo kukusanya kiasi cha Sh. Bilioni
37 na kuongeza kuwa hiyo ni changamoto kubwa kwao.
Kaliza alisema mwaka
uliopita mkoa wa Dodoma ulipangiwa kukusanya jumla ya Sh. bilioni
24.5 sawa na asilimia 93.5 huku lengo likiwa ni kukusanya bilioni 26.
Aidha alisema ongezeo
hilo la mwaka huu, TRA kutakiwa kukusanya Sh. bilioni 37 ni sawa na
asilimia 10.
Alisema Watanzana wengi hawajisikii fahali kulipa kodi
kwa faida ya maendeleo ya Taifa na badala yake wanaona ufahali kukwepa kulipa
kodi.
Aliwataka
Watanzania kujenga utamaduni wa kudai risiti pindi wanaponunua bidhaa
mbalimbali ili kusaidia Nchi kukusanya mapato.
Alisema taaluma ya kodi ina changamoto nyingi lakini cha
msingi ni kuangalia jinsi gani walipa kodi wanavyoangalia suala hilo na lina
faida gani kwao.
Alisema ni muhimu kwa wafanyabiashara kuwa na mashine
unakuwa na uhakika na kile unachokipata katika biashara.
No comments:
Post a Comment